Jumanne , 16th Jul , 2024

Washiriki wa Mashindano ya Kombe la Mkuu wa Majeshi, (CDF 2024) wameendelea na matayarisho kabambe kuelekea kwenye uzinduzi wa mashindano hayo yanayotaraji kuanza Julai 20-2024 kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam

Wakizungumza na EATV, Mabondia watakaoshiriki kwenye shindano hilo wametamba kuchukua medali  katika mashindano hayo ambayo yatahusisha kamandi zote za Jeshi hapa nchini.

Kwa upande mwingine,Wakufunzi kutoka kamandi Mbalimbali  Jeshini kwa upande wa mchezo wa  Masumbwi wameelezea umuhimu wa mashindano hayo ya mkuu wa Majeshi CDF 2024 kuwa yanatengeneza nidhamu na kuinua vipaji vya michezo kwa wanajeshi .

Mashindano ya Mkuu wa Majeshi CDF CUP Yalianzishwa  na Mkuu wa majeshi Mstaafu Jenerali Davis Mwamunyange mwaka 2014 huku mara ya mwisho kufanyika ilikuwa mwaka 2018.