
wachezaji wa Simba wakishangilia ushindi wao.
Mhe. Mchengerwa ametoa pongezi hizo, baada ya kumalizika kwa mpambano huo ambapo amesema ushindi huo ni ushindi wa kihistoria.
"Ninaipongeza timu ya Simba kwa ushindi wa kishindo kuelekea kwenye robo fainali ya mashindano ya shirikisho la mpira wa miguu la Afrika. kama taifa, tunajivunia kwa ushindi huo mnono unaoitangaza nchi yetu kimataifa." amesema Waziri Mchengerwa.
Vilevile waziri Mchengerwa ameitaka timu ya Simba kufanya maandalizi ya kutosha ili kuweza kufanya vizuri zaidi katika mashindano hayo hatimaye kuchukua kombe na kuendelea kuitangaza Tanzania duniani.
Simba kwenye michuano ya robo fainali inaweza kukutana na TP Mazembe(DR Congo), Orlando Pirates ( Afrika Kusini) na Al Ahly Tripoli (Libya).
Ukiachilia timu hizi nne(4) timu nyingine nne(4) ambazo zimefuzu kuingia robo fainali ya mashindano haya ni pamoja na RS Berkane (Morocco), Pyramids (Misri), Al-Ittihad (Libya) na Al Masry Misri.
Simba inatarajiwa kuanzia nyumbani Uwanja wa Mkapa.