Jumanne , 29th Jun , 2021

Bingwa mara tano wa michuano ya Wimbledon , Serena Williams ameanza vyema mashindano hayo kwa ushindi Mihaela Buzarnescu na kufuzu raundi ya kwanza.

Bingwa mara 5 wa michuano wa Wimbledon, Serena Williams akiwa uwanjani.

Serena mwenye umri wa miaka 41, anashiriki michuano hiyo kwa mara ya 23 na ni ushindi wake wa 90 katika mashindano hayo.

Nyota huyo ambaye kwasasa anashikilia nafasi ya 111 kwenye viwango vya ubora duniani kwa wanawake, atacheza dhidi ya Ons Jabeur katika raundi ya pili.

Kwa mara ya kwanza kushiriki michuano hiyo ilikuwa mwaka 1997, lakini akatwaa ubingwa wake wa kwanza wa miaka mitatu iliyofuatia.