Jumatano , 13th Oct , 2021

Mkurugenzi Mtendaji wa timu ya Brooklyn Nets, Sean Marks amesema hali ilivyo kwasasa mchezaji wao nyota Kyrie Irving hatoweza kufanya mazoezi ya pamoja na wachezaji wenzake na hata kuhusishwa kwenye masuala ya timu kwasababu bado hajapata chanjo ya Covid-19.

Nyota wa Brooklyn Nets, Kyrie Irving.

Sean amesema, “Kwasasa uamuzi wake una mzuia kuwa na timu katika mazingira yote. Na hatutomruhusu mtu yeyote wa timu yetu kushiriki nusu nusu. Kulingana na hali ilivyo, Kyrie Irving hatocheza walal kufanya mazoezi na timu mpaka atakapokuwa mchezaji halali kuruhusiwa kucheza”.

Msimamo huo wa Brooklyn umekuja baada ya sheria na taratibu za mji wa New York kusomeka kuwa, wachezaji na watu mashuhuri weengine ni lazima wachanje ili wahusike kwenye mikusanyiko na hata kwenye michezo yao ya ligi mbali mbali ikiwemo Covid-19.

Ikumbukwe kuwa Irving aliweka wazi msimamo wake juu y chanjo ya Covid-19 na kusema, “Mimi ninalindwa na Mungu, pamoja na watu. Tunasimama pamoja”.

Tyari Kyrie amekosa michezo mitatu ya NBA Pre-season ukiwemo ushindi wa kibabe mbele ya wapinzani wao Los Angeles Laker.