Alhamisi , 16th Sep , 2021

Mambo yamezidi kuwa magumu kwa mchezaji wa Tenisi, Andy Murray baada ya kutupwa nje kwenye hatua ya 16 bora katika mashindano ya Rennes Open yanayoendelea nchini Ufaransa.

Andy Murray akiokoa mpira kwenye mchezo wa usiku wa jana.

Seti 6-2, 4-6,6-1 hazikumtosha Muingereza huyo kumshinda Roman Safiullin kutoka nchini Urusi ambaye anashika nafasi ya 163 kwenye viwango vya ubora ulimwenguni kwenye mchezo huo, ambaye anashikilia rekodi ya kuwa mchezaji mwenye umri mdogo kuwahi kushinda mashindano ya Australian Open 2015.

Kwa upande wa Murray atakuwa na nafasi nyingine wiki ijayo, kusahihisha makosa yake kwenye michuano inayofahamika kama Metz Open.

Ikumbukwe Murray anashikilia rekodi ya kushinda mataji matatu ya Grand Slam, yakiwemo ya Wimbledon (2013, 2016) pamoja na US Open (2012).