Mane amejiunga na klabu hiyo kwa mkataba wa miaka mitano, ni mchezaji watatu kusajiliwa katika kipindi cha kiangazi baada ya kipa Mjerumani Loris Karius na beki Mkameruni Joel Matip.
Mchezaji huyo raia wa Senegal mwenye umri wa miaka 24 alifunga magoli 21 katika mechi 67 za Ligi Kuu kwa Southmpton, baada ya kijiunga nao kwa uhamisho wa paundi 10 kutoka Salzburg mwaka 2014.
Mane amesema amefurahishwa zaidi kwa kujiunga na moja ya vilabu vikubwa barani Ulaya.



