Jumatano , 1st Dec , 2021

Chombo cha Habari ‘Telefot’ cha nchini England kimetoa taarifa za kikachero kwa kueleza sababu za kwanini Mauriccio Pochettino alishindwa kujiunga na Manchester United kuchukua mikoba ya Ole Gunnar Solskjear mwezi uiopita.

(Kocha wa PSG, Mauriccio Pochettino)

Telefoot lmeeleza kuwa, moja ya sababu ni masuala ya fedha. PSG inaelezwa ilikuwa tayari kuruhusu Machester United iongee na Pochettino na kumchukua kama watakuwa tayari kutoa Euro milioni 15-20.

Fedha hizo ni sawa na bilioni 39 na zaidi ya milioni 65za Kitanzania jambo ambalo linaelezwa Mashetani wekundu hawakuwa tayari kuitoa. Sababu ya pili inaelezwa ni PSG kupata mashaka ya mbadala wa Pochettino kwa uharaka.

Telefoot wamepapambanua kuwa, PSG walifikiria na kuona kwa muda ule isingekuwa rahisi kumpata kocha ambaye angeweza kuishi wa wachezaji wao nyota kikosini na kuwapa matokeo.

Baadhi ya wachezaji nyota kwenye kikosi cha PSG ni Lionel Messi, Kylian Mbappe, Neymar JR, Sergio Ramos, Angel Di Maraia, Gianluigi Donnarumma na Marco Verratti na wengine wengi jambo ambalo Pochettino linampa ugumu.

Kwasasa, Manchester United wapo na kocha wake wa muda hadi mwisho wa msimu huu, Ralf Hangnick na mkataba huo mfupi ukimalizika basi atasalia old Trafford ili awe Mshauri wa masuala ya ufundi wa klabu hiyo.