Alhamisi , 1st Jul , 2021

Uongozi wa klabu ya KMC 'Kino Boys' umesema mchezo wake dhidi ya Simba kwenye Ligi kuu Bara utachezwa kwenye dimba la Benjamin William Mkapa Julai 7 mwaka huu baada bodi ya Ligi kurithia ombi la KMC kutumia uwanja huo kama uwanja wake wa nyumbani.

Kikosi cha KMC cha msimu wa huu wa mwaka 2020-2021.

KMC imetumia kanuni ya ligi inayowaruhusu kuchagua kwa awamu mbili kuchagua viwanja kuvitumia kama viwanja vyake vya nyumbani baada ya kupeleka maombi na kukubaliwa na bodi hiyo.

Khatibu wa KMC, Walter Harison amethibitisha kwa kusema;

“Mchezo wetu huo utachezwa kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa 7,7,2021 kwahyio ombi letu ambalo tulilolipeleka bodi ya ligi limeweza kukubaliwa hivyo mchezo huo umehama rasmi na ijulikane hivyo na mashabiki wajitokeze kwa wingi kwa ajili ya kutuunga mkono”

Harison pia amezungumzia malengo ya msimu ya klabu hiyo kwa msimu huu kwa kusema;

“Tunaelekea mwishoni mwa ligi na tuna malengo ya kuhakikisha kuwa tunafanya vizuri na kupata nafasi za juu kwenye ligi na ndoto yetu ni kuona jinsi ambavyo tunaweza tukafanya kupata nafasi ya kuiwakilisha nchi kwenye michuano ya kimataifa hasa ukizingatia kwamba msimu unaofuata wa michuano ya Afrika nchi yetu itatoa timu nne ambazo zitashiriki kwenye michuano hiyo” 

“Kwahiyo tunaomba washabiki wajitokeze kwa wingi kabisa kwenye mchezo huo dhidi ya Simba tunaamini kabisa itakuwa siku nzuri ya siis kuweza kupata ushindi utakaotuweza vizuri kwenye msimu wa ligi na kuweza kutimiza malengo tuliyojiwekea”

KMC ipo nafasi ya 6 ikiwa na alama 42 ilhali Simba ndiyo kinara wa ligi hiyo ikiwa na alama 73 baada ya michezo 29.