Jumatano , 20th Jul , 2016

Timu ya soka ya Ruvu Shooting ya Mkoani Pwani imeachana na kocha wake Tom Olaba raia wa Kenya,pamoja na Kocha huyo kuiridisha timu hiyo Ligi Kuu bara.

Aliyekuwa kocha wa Ruvu Shooting, Tom Olaba

Mikoba ya Olaba sasa amekabidhiwa kocha mzawa Selemani Mtingwe aliyemaliza mafunzo ya ukocha ya leseni daraja B hivi karibuni.

Afisa Habari wa Ruvu Shooting, Masau Bwire amesema wanaheshimu sana mchango wa Olaba katika timu hiyo na wanamheshimu sana Olaba na wataendelea kumheshimu na kuamini kuwa ni miongoni mwa makocha bora katika ukanda huu wa nchi za maziwa makuu na Afrika.

Olaba alijiunga na Ruvu Shooting msimu wa mwaka 2013/14 mzunguko wa pili baada ya aliyekuwa Kocha Mkuu Boniphace Mkwasa kuvunja mkataba na kujiunga na Yanga.

Msimu wa 2014/15 Ruvu Shooting ilishuka daraja chini ya Olaba lakini amefanikiwa kuirudisha ligi kuu.