Timu mojawapo iliyokabidhiwa vifaa ni timu ya riadha ya JWTZ inayokwenda kushiriki mashindano ya Majeshi (CISM) nchini Uswiss tarehe 29 na 30 Oktoba 2023.
Makabidhiano hayo yalifanywa na Katibu Mkuu wa Shirikisho hilo wakili Jackson Ndaweka katika uwanja wa Shekh Amri Abeid Kaluta jijini Arusha.
Akipokea vifaa hivyo kwa niaba ya Mkuu wa Majeshi, Kamanda wa Kikosi cha 977 Col Khamis Kinguye amelishukuru shirikisho hilo na kuwataka wachezaji kutendea haki heshima waliyopewa.
“ninawahakikishia wachezaji wote kwamba Jeshi na nchi kwa ujumla tuko pamoja nanyi, nendeni mkapambane , muwe wazalendo na kufanya Juhudi binafsi ili tusimuangushe Amiri Jeshi Mkuu na Rais wetu wa Nchi Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan “ alisisitiza Col H. Kinguye.
Wachezaji waliokabidhiwa vifaa hivyo wanaokwenda mbio za majeshi ni Alphonce Felix Simbu, Joseph Panga , Faraja Lazaro Damas, Magdalena Shauri, Mayselina Mbua na Jackline Sakilu huku wakiongozwa na Meneja wa Timu Capt. Christopher Massanga na Kocha Mkuu ni Anthony Mwingereza
Kwa wanariadha wanaokwenda Nagai City Marathon tarehe 15/10/2023 na kukabidhiwa vifaa hivyo ni Josephat Gisemo, Fabiano Joseph, na Peter Sulle.Wengine ni Paul Damian , Sarah Ramadhani na Transfora Musa , huku kocha akiwa ni Samsoni Ramadhani na kiongozi wa msafara ukiongozwa na Col. (Mst) Juma R. Ikangaa.