Jumatano , 16th Dec , 2015

Timu ya Taifa ya Tanzania ya mchezo wa Roll Ball imeitaka Serikali pamoja na wadau wa michezo kuweza kusimamia michezo mbalimbali nchini ambayo inashiriki mashindano makubwa ya kuweza kuitangaza nchi.

Nahodha wa timu hoyo Feruzi Juma amesema, wameshindwa kushiriki mashindano ya Kombe la Dunia ya mchezo huo yaliyoanza rasmi hii leo nchini India kutokana na ubalozi wa India kushindwa hadi hii leo kuwakamilishia suala la visa.

Feruzi amesema, katika mashindano hayo gharama za safari kwa timju zimetolewa na chama cha dunia cha mchezo huo ambapo wao kama timu walianza kuhangaikia masuala yote ya safari lakini wameshangaa ubalozi kuanza kuwazungusha katika suala la visa ambapo hadi wizara ya michezo imeingilia kati lakini bado imeshindikana.

Feruzi amesema, wameenda mpaka ubalozi wa Asia pia balozi akatoa kauli ili timu hiyo iondoke ikashindikana na mpaka hivi leo bado wapo nchini na wameshindwa kushiriki mashindano hayo.