Kocha Severin Luthi (kushoto) akiwa na Rodger Federer
Imekuwa ikiripotiwa kuwa raia huyu wa Uswiss ambaye mwezi August atakuwa anafikisha miaka 39 alipanga kustaafu mwaka huu 2020 baada ya michuano ya Olympic, lakini michuano hiyo hakufanyika kutokana na dharula ya mlipuko wa Corona.
Kocha Luthi ambaye amekuwa na Federer toka mwaka 2007 amekanusha taarifa hizo na kusema mchezaji wake ambaye anaongoza kwa kutwaa mataji mengi ya Grand Slam kwa wanaume katiksa historia ya mchezo hu anajipanga kurejea kwenye mashindano mwakani kutokana na kuwa na majeraha ya goti.
Rodger Federer atakaa nje ya uwanja kwa kipindi chote kilichobaki mwaka huu baada ya kufanyiwa upasuaji wa goti lake la kulia. Mwaka huu mwezi January Federer alifanikiwa kufika hatua ya nusu fainali ya michuano ya wazi ya Australia kabla ya kutolewa na Novac Djokovic katika hatua hiyo.
Kalenda ya mashindano ya Tenisi mwaka huu ilishindwa kwenda kama ilivyopangwa kutokana na mlipuko wa virusi vya Corona na inaripotiwa mwezi August mchezo huu utanza kuchezwa tena.




