Jumatatu , 14th Aug , 2023

Kocha Mkuu wa Simba SC Roberto Oliviera ‘Robertinho’ ameelezea furaha yake ya kuchukua taji la kwanza tangu aanze kukinoa kikosi chetu.

Robertinho amesema ameshinda mataji mbalimbali katika timu alizozifundisha awali ila ndani ya kikosi cha Ngao ya Jamii waliyoipata  kwa kuifunga Yanga kwa mikwaju ya penati 3-1 ndio la kwanza.

Robertinho ameongeza kuwa haikuwa rahisi kushinda lakini amewapongeza wachezaji kwa kujituma hadi mwisho ili kufanikisha.

“Nina furaha kupata taji langu la kwanza hapa, ni jambo kubwa ambalo linatupa dira kuelekea msimu mpya wa mashindano.

“Nimechukua mataji matatu nikiwa Rwanda na matatu nikiwa Uganda lakini kwa hapa Tanzania hili nilakwanza. Nawapongeza wachezaji, benchi la ufundi na viongozi kwa kufanikisha hili,” amesema Robertinho.

Robertinho amewapongeza mashabiki  kwa kuendelea kuisapoti timu kila inapokuwa na imekuwa chachu kubwa ya wachezaji kujituma uwanjani kuhakikisha wanapata  matokeo chanya.

“Nawapongeza mashabiki wetu, wanaipenda sana timu yao. Mara zote wanajitokeza kwa wingi uwanjani kila timu inapokuwa, hili linaongeza hamasa kwa wachezaji,” amesema Robertinho.

Mabingwa hao wa ngao jamii Simba SC watacheza mchezo wa kwanza wa Ligi kuu  wakiwa ugenini dhidi ya Mtibwa Sugar mnamo Agosti 17 ,2023 katika dimba Uwanja wa Manungu uliopo Morogoro