Jumanne , 19th Mei , 2015

Uongozi wa Timu ya Mtibwa Sugar ya Mjini Morogoro umesema unasubiri ripoti ya Kocha wao, Mecky Mexime kabla yua kuanza usajili wa msimu uajo wa Ligi kuu ya Soka Tanzania Bara.

Akizungumza na East Africa Radio, Afisa habari Thobias Kifaru amesema timu hiyo itaanza usajili wake baada ya ripoti ya Mexime kutua mezani kwao na kuijadili.

Kifarua amesema, uongozi wa timu hiyo una imani na benchi lake la ufundi na ndiyo maana wanasubiri mapendekezo yake ili wajue wapi wanatakiwa kufanya marekebisho ili kukiboresha zaidi kikosi hicho na kufanya mabadiliko makubwa katika ligi hiyo ambayo anaamini itakuwa na ushindani mkubwa kutokana na timu kuongezeka.

Kifaru amesema, uongozi wa klabu hiyo umepanga kubakia na wachezaji wake wote waliomaliza ligi na tayari wameanza mazungumzo nao ili kujua matatizo waliyonayo.

Mtibwa ilimaliza ligi ikiwa katika nafasi ya saba licha ya kuanza msimu vizuri ikiwamo kukalia Uongozi.