Ijumaa , 6th Aug , 2021

Rais wa klabu ya Barcelona, Juan Laporta amesema uongozi wa klabu hiyo ulifanya kila liwezekanalo pamoja na kambi ya mchezaji wake Lionel Messi ili kumbakisha mchezaji huyo klabu hapo lakini ilishindikana kutokana na kanuni za La Liga juu ya uwiano mzuri wa mapato na matumizi ya klabu.

Lionel Messi (kushoto) na rais wa Barcelona, Juan Laporta (kulia).

Laporta ameyasema hayo mchana wa leo Agosti 6, 2021 wakati alipokuwa anazungumza na wanahabari juu ya taarifa za kushtukiza za Messi kuondoka kwenye klabu hiyo jambo ambalo halikutegemewa na wapenzi wengi wa klabu hiyo ukizingatia wiki mbili zilizopita iliripotiwa kuwa Messi na Barcelona walifikia makubaliano ya kusaini mkataba wa miaka mitano hadi 2026.

Laporta amesema; “Messi alitaka kusalia Barcelona, alikuwa na makubaliano ya kubaki Barca na tulitaka Messi abaki. Ninapenda kuishukuru kambi ya Leo Messi na watu wote waliohusika katika majadiliano. Kwa bahati mbaya, kwa sababu ya kanuni za La Liga hatuwezi kuendelea”.

"Mazungumzo na Leo Mess yamefka tamati. Hatuwezi +kumsajili Mess kwasaabu ya kanuni za La La Liga, haziwezi kubadilika kwetu katika ukomo wa mshahara ukizingatai tulikuwa na ukomo wa terehe ya kulikamilisha hilio”.

Akijibia uwezekano wa klabu hiyo kulitatua sakata hilo, Laporrta amesema; “Hatuwezi kuwapap matumaini ya uongo washabiki wetu, inabidi tusonge mbele. Barecelona itakuwa juu ya kila kitu”., 

Messi ataondoka Barcelona akiwa mchezaji shujaa wa muda wote baada ya kuhezo michezo 778, kufunga mabao 672 na kuassist mabao 305, Messi ameweka rekodi ya kuwa mchezaji pekee aliyehusika kwenye mabao mengi, mabao 977 na kushinda mataji mengi, mataji 35 pamoja na  tuzo 6 za mchezaji bora wa Dunia.