Mlinzi wa Liverpool Dejan Lovren (Kushoto), akijarimu kuamua ugomvi kati ya Joe Gomez (Kulia) na Raheem Sterling (Kati kati) katika moja ya mechi zilizowakutanisha.
Mabao ya Arsenal yalifungwa na Alexandre Laccazete dakika ya 32 na Reiss Nelson dakika ya 44 wakifuta uongozi wa Liverpool ambao walipata bao la mapema na Sadio Mane aliyefunga dakika ya 20,na sasa vijana wa Jurgen Klopp wenye alama 93 hawatoweza kufikisha alama 100 hata kama watashinda mechi tatu zilizosalia.
Akizungumza mara baada ya mchezo kumalizika, kocha wa Liverpool Jurgen Klopp amesema wanapaswa kujifunza kutokana na makosa ambayo yamesababisha kuadhibiwa katika mechi za hivi karibuni.
Mlinzi wa Liverpool Virgil Van Dijk alifanya makosa yaliyomuwezesha Lacazette kumpora mpira katika eneo la hatari na kusawazisha bao, pia mlinda mlango Allison Becker alishindwa kuondoa mpira dakika ya 44 iliyopelekea Nelson afunge bao la 2.
Ushindi huo kwa Arsenal ni wa kwanza dhidi ya Liverpool tangu mwaka 2015 na ni kwa mara ya kwanza kocha Jurgen Klopp kufungwa na The Gunners ambapo kabla alikua ameshinda mechi 5 na sare 3.
Liverpool itakabidhiwa taji lake la EPL siku ya Jumatano ijayo mara baada ya mchezo wao dhidi ya Chelsea utakaopigwa uwanjani Anfield.




