
Wachezaji wa Liverpool
Katika mchezo wa jana Disemba 26, 2019 dhidi ya Leicester City, Liverpool wameweka rekodi 6 tofauti baada ya kuibuka na ushindi wa magoli 4-0 ugenini.
1. Kwa mara ya kwanza Liverpool wameshinda mechi 5 mfululizo zilizochezwa Boxing Day. Wakiwa wameshinda jumla ya magoli 15-0 katika mechi hizo tano, ikiwemo ya jana dhidi ya Leiceter City.
2. Ushindi wa Liverpool wa magoli 4-0 dhidi ya Leicester City, ulikuwa ndio ushindi mkubwa zaidi kati ya timu mbili za juu kwenye msimamo, tangu Manchester City ilipokuwa inaongoza ligi, ilipoifunga Manchester United iliyokuwa nafasi ya pili kwa magoli 6-1 mwaka 2011.
3. Goli la pili la Roberto Firmino na la tatu kwa Liverpool dhidi ya Leicester City jana, lilikuwa goli la 500 kwa Liverpool chini ya Jurgen Klopp katika mashindano yote.
4. James Milner baada ya penalti ya jana sasa amefunga mikwaju ya penalti 17 kati ya 19 ailiyopiga kwenye Premier League. Kati ya hizo, 14 ni ndani ya Liverpool na amefunga 13 na kukosa 1 tu.
5. Tangu ulipoanza msimu wa 2018/19 hadi huu wa 2019/20 mchezaji Trent Alexander-Arnold ametengeneza magoli 20 ambayo ni zaidi ya mchezaji yoyote.
6. Magoli 8 ya mwisho ya Mshambuliaji wa Kibrazil Roberto Firmino kwa Liverpool katika michuano yote, amefunga nje ya uwanja wa Anfield.