Jumatatu , 11th Jun , 2018

Wakati dirisha la usajili likiendelea kuwa wazi barani Ulaya, tetesizinaeleza kuwa Rais wa Klabu ya Bayern Munich, Uli Hoeness amesema hawana mpango wa kumuuza straika wao, Robert Lewandowski.

Kumekuwa na habari kuwa kwa pauni milioni 176 mshambuliaji huyo ataingizwa sokoni baada ya kuitumikia klabu hiyo kwa miaka kadhaa tangu alipotokea Borussia Dortmund.

Uli amesema madai hayo ni ya uongo na hakuna mpango kama huo wa kumuuza Lewandowiski ambaye ana umri wa miaka 29.

 Manchester United na Chelsea zinatajwa kumuwania huku pia Real Madrid nayo ikihusiswa.