Jumanne , 6th Jan , 2015

SHIRIKISHO la Ngumi Tanzania PST limesema kwa mwaka huu limeandaa mapambano mengi yatakayoweza kuwasaidia mabondia kuweza kufanya vizuri katika mapambano mbalimbali makubwa yatakayotokea nje ya nchi.

Akizungumza na East Africa Radio, Katibu mkuu wa wa PST, Antony Rutha amesema mwaka jana walipata bahati mbaya kwa mabondia kushindwa kufanya vizuri kutokana na kutokuwa na maandalizi ya kutosha hususani kutokuwa na mapambano mengi ya majaribio ambayo yangeweza kuwasaidia kuweza kupambana wakiwa na mapambano mengi waliyopambana kabla ya mapambano makubwa.

Rutha amesema, Januari 31 Mohamed Matumla atapanda ulingoni kupambana na Bondia anayepambana mapambano ya kulipwa nchini Kenya, Emilio Novert huku wakusindikizwa na Pambano la kuwania Ubingwa wa Afrika litakalowakutanisha Nassib Ramadhan na Issa Nampepeche.

Rutha amesema, Februari 28 kutakuwa na pambano lingine la kuwania Ubingwa wa Afrika litakalowakutanisha Cosmas Cheka na Ibrahim Class, huku Machi 29 wakiwakutanisha Mada Maugo na Kalama Nyilawila.

Rutha amesema, wanaimani mapambano hayo yataweza kuwapa nguvu ya kuweza kupambana na kuweza kushinda katika mashindano mbalimbali na kuweza kuipeperusha bendera ya Taifa.