
Mshambuliaji wa Azam, Prince Dube akishangilia bado baada ya kuifunga Yanga miezi miwili iliyopita.
Dube amesema “Ni jambo linalohusu hulka na kwenda pale kupambana kwa ajili ya nembo ya timu, kupambana kwa ajili ya Azam”.
“Unajua mashabiki wetu wamekuwa wakituunga mkono sana katika kipindi kizuri na kibaya, sasa ni wakati wetu kuwalipa kile ambacho wamekuwa wakikitoa kwetu sisi wachezaji”.
Kwa upande wa Mkuu wa Idara ya Habari na Mahusiano wa klabu ya Azam, Zakaria Thabiti 'Zaka Zakazi' amesema wachezaji wote wa wanalamba lamba hao wapo fiti kuwavaa Rhino Rangers ya mkoani Tabora anaamini ubora wa kikosi hicho kitawafanya waibuke kidedeana kutinga nusu fainal
Mshindi wa mchezo wa Azam dhidi ya Rhino Rangers kwenye dimba la CCM Kambarage mkoani Shinyanga atacheza na mshindi wa mchezo kati ya Simba na Dodoma Jiji huku Yanga ambaye jioni ya jana aliibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mwadui watacheza na Biashara United Mara.