Kikosi ch polisi Tanzania katika picha ya pamoja
Wakiongea na EATV leo katika Uwanja wa Uhuru Dar Es Salaam manahodha wa kikosi hicho Pato Ngonyani na Shaabani Stambuli wamesema maandalizi yao ni mazuri kuelekea mchezo huo .
"Wachezaji wetu 20 waliosafiri kikosini wote wako imara, tumemaliza mazoezi salama na tunawasubiri Yanga siku ya kesho na kiukweli hatuwaogopi ila tunawaheshimu" amesema Stambuli.
Katika michezo mitatu ya hivi karibuni timu hizo zimetoka sare mara mbili na mchezo mmoja, Polisi Tanzania waliibuka kifua mbele dhidi ya Yanga ikiwa ni wa kirafiki.
Aidha, msimamo wa VPL unaonesha Yanga wakiwa nafasi ya tatu wakijikusanyia alama 13 katika mechi tano huku Polisi Tanzania wakiwa na alama 11 katika mechi sita wakishikilia nafasi ya 7 kwenye msimamo.