Jumatano , 8th Nov , 2023

Beki wa FC Porto Pepe ameweka rekodi ya kuwa mchezaji mwenye umri mkubwa zaidi kufanga bao kwenye michuano ya Ligi ya mabingwa barani Ulaya (UEFA Champions League) baada ya kufunga bao la pili la FC Porto kwenye ushindi wa mabao 2-0 walioupata dhidi ya Royal Anterwap jana usiku.

Pepe ameweka rekodi ya kuwa mchezaji mwenye umri mkubwa zaidi kufunga bao kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya, akiwa na umri wa miaka 40 na siku 254.

Pepe amefunga bao hilo akiwa na umri wa miaka 40 na siku 254 akivunja rekodi ya mshambuliaji wa zamani wa AS Roma Francesco Toti ambaye alifunga bao kwenye michuano hiyo akiwa na umri wa miaka 38 na siku 59. Kwa upande mwingine msimu huu Pepe ndio mchezaji mwenye umri mkubwa zaidi anayecheza kwenye michuano hii ya ligi ya mabingwa Ulaya.

Pepe ameweka rekodi hii akiwa amecheza michezo 115 ya michuano hiyo akiwa na vilabu vya Real Madrid, FC Porto na Besiktas. Kwa ujumla mpaka sasa akiwa na umri wa miaka 40 Pepe kwa ujumla amechrza michezo 714 kwenye maisha yake ya soka na kafunga mabao 40