Jumatatu , 30th Jan , 2017

Timu ya Taifa ya Misri usiku wa jana imetimiza orodha ya timu nne ambazo zinayapeleka mashindano ya Mataifa Afrika (AFCON 2017) katika hatua ya nusu fainali ikiungana na Ghana, Burkina Faso na Cameroon.

Mechi za nusu fainali zinapigwa Februari 01, hadi Februari 03, ambapo nusu fainali ya kwanza itakuwa ni kati ya Burkina Faso na Misri Jumatano ya Februari 01, saa 4 usiku wakati nusu fainali ya pili ikiwa ni ni Alhamis Februari 02 kati ya Cameroon na Ghana 

Misri imetinga hatua hiyo kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Morocco, katika dakika ya 88 kupitia kwa Kahraba baada ya kubanana vilivyo katika dakika zote za mchezo uliokuwa wa ngunvu na wenye ushindani wa aina yake.

Kwa upande wa Ghana ambao nao wapenya katika hatua hiyo siku ya jana ambapo ndugu wawili Jordan na Andre Ayew walifunga bao moja moja na kuisaidia timu hiyo kuitoa DR Congo kwa mabao 2-1 na kuivusha Black Stars.

Jordan Ayew anayechezea Aston Villa ya ligi kuu ya soka nchini Unigereza, alifunga bao la kuongoza kunako dakika ya 62, kabla ya Paul-Jose M'Poku kufanya jitihada binafsi na kufunga bao la mpira mrefu kutoka nje ya box, kwenye dakika ya 68.

Lakini Andre Ayew aliifungia Ghana bao la pili kwa njia ya penati kunako dakika ya 78, na kumchambua mlinda mlango wa Congo, Ley Matampi, akipotea golini.

Cameroon wao waliwatoa Senegal kwa mikwaju ya penati baada ya kutoshana nguvu katika dakika zote 120 kwa bila kutoka 0-0 ambapo mshambuliaji tegemeo wa Senegal na Liverpool Sadio Mane alikosa penati yake na kufanya huku Cameroon wakipata zote 5.

Burkina Faso wao walitinga hatua hiyo baada ya kuichapa Tunisia mabao 2-0.