Ijumaa , 9th Feb , 2018

Klabu ya soka ya Singida United imethibitisha kurejea kwa nyota wake Dany Usengimana ambaye alikuwa nje ya uwanja kutokana na kuumia katika moja ya mechi za ligi kuu hivi karibuni.

Usengimana ambaye ni raia wa Burundi amerejea leo kwenye mazoezi ya timu hiyo na kuendelea na maandalizi ya mchezo wao ujao wa ligi kuu dhidi ya Stand United ya Shinyanga.

Singida United imekuwa ni moja ya timu tishio kwenye ligi kuu ambapo hadi sasa imejikusanyia alama 33 katika nafasi ya nne sawa na Azam FC yenye alama 33 zikitofautiana mabao ya kufunga na kufungwa.

Kwa upande mwingine timu hiyo bado haijatoa taarifa kama imeshampunguzia adhabu nyota wake, Kambale Salita Gentil ambaye alisimamishwa kwa muda usiojulikana kwa utovu wa nidhamu uwanjani japo alikiri kosa na kuomba msahama.