Jaylen Brown kushoto na Jayson Tatum
Wachezaji hao wamefikia rekodi hiyo baada ya kukiongoza kikosi cha Boston Celtics kushinda mchezo wa 3 wa fainali ya Ligi ya mpira wa kikapu nchini Marekani NBA Alfajiri ya leo kwa kuifunga Golden state worriors kwa alama 116 kwa 100 na kuongoza 2-1 katika michezo 3 iliyochezwa katika mfululizo wa michezo 7 ya Fainali.
Kwenye mchezo huu wachezaji hao watatu wa Boston Celtics wamefunga juu ya alama 20, ambapo Jason Tatum amefunga alama 26 ametoa pasi za kufunga (Assist) 9 na Rebound 6 Jaylen Brown amefunga alama 27 pasi za kufunga (Assist) 5 na Rebound 9 nae Murcus Smart amefunga alama 24 pasi za kufunga (Assist) 5 na Rebound 7.
Kwa upande wa Golden State worriors mchezaji nyota wa timu hiyo Stephen Curry amefunga alama 31 pasi za kufunga (Assist) 2 na Rebound 4, na Klay Thompson amefunga alama 25 pasi za kufunga (Assist) 3 na Rebound 3.



