Alhamisi , 14th Sep , 2023

Kikosi cha wachezaji 23 kimeondoka jijini Dar es Salaam mchana kuelekea Zambia tayari kwa mchezo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Power Dynamos.

Kikosi kimeondoka na benchi zima la ufundi likiongozwa na kocha Mkuu Roberto Oliviera ‘Robertinho’.

Baada ya kufika Zambia kikosi kitafanya mazoezi ya mwisho kesho jioni katika Uwanja wa Levy Mwanawasa ambao tutautumia kwa mchezo wetu wa Jumamosi.

Wameondoka nchini Tanzania  wakiwa  na matarajio kikabo ya kufanya vyema  kwenye mchezo huo  mgumu na wanaiheshimu  Power Dynamos lakini wamejipanga  kufanya vizuri.

Huku wakiingia  kwenye mchezo wakiwa  na lengo moja la kutafuta ushindi kwenye mchezo wa ugenini ili kujiweka kwenye mazingira mazuri katika mechi ya mkondo wa pili utaopigwa jijini Dar es salaam.