Jumatatu , 11th Jun , 2018

Muda mfupi baada ya kuelezwa kuwa Klabu ya Yanga imemshusha nchini straika Marcellina Koupko kutoka Benin, mashabiki wa timu hiyo wamendeelea kumuulizia beki wa kati Juma Nyosso.

Ilidaiwa kuwa Yanga ipo katika harakati za kumsajili Nyosso kutoka Kagera Sugar ili kuongeza nguvu kikosini hapo baada ya kuyumba kwenye idara ya ulinzi msimu uliopita.

Nyosso ni beki mkongwe ambaye aliwahi kutamba akiwa Simba lakini mara kadhaa amejikuta akiingia kwenye mikwaruzano na viongozi wa soka kutokana na tabia za utovu wa nidhamu.

Pamoja na hayo yote bado mashabiki wa Yanga wanaamini Mchezaji huyo anaweza kuwasaidia hasa kipindi hiki ambapo Kelvin Yondani ndiye ameonekana kukosa pacha mzuri wa kucheza naye.

Nyosso na Yondani waliwahi kucheza pamoja katika klabu ya Simba kabla ya wote kutimkia vilabu tofauti. Yondani alikwenda Yanga huku Nyoso akitua Mbeya City kabla ya kwenda Kagaera Sugar.