Akizungumza na East Africa Radio, Nyambui amesema, kwa umri alionao alitamani kumalizia majukumu yake hapa nchini ili kuendelea kufanya mabadiliko zaidi kwa upande wa riadha.
Nyambui amesema, kinachomsikitisha ni suala zima la kuondoka lakini bado anatamani kufanya mabadiliko mazuri ambayo yatafanya riadha ya Tanzania kufanya vizuri katika mashindano makubwa ya ndani na nje ya nchi.
Nyambui amesema, mpaka sasa Tanzania hakuna kituo wataalamu wa michezo wa kutosha suala ambalo mpaka sasa halijafahamika.
Nyambui amesema, hakuna kituo mahususi cha kuweza kuandaa timu chenye wataalamu wa hali ya juu ambao sio makocha pekee ambao wataangalia hali ya mchezaji iko vipi.
Nyambui ameachia ngazi ukatibu mkuu wa RT baada ya kupata kazi ya kuwa kocha mkuu wa Brunei pamoja na mshauri wa wizara ya michezo nchini humo ambapo anatarajiwa kuondoka Jumatano ya wiki hii kuelekea nchini humo kwa ajili ya kuanza kazi.