Jumamosi , 21st Jan , 2023

Novak Djokovic amefuzu kwenye mzunguko wa 16 wa michuano ya wazi ya tenisi ya Australia 2023 baada ya kumfunga Mbulgaria Grigor Dimitrov kwa seti 3-0 yaani (7-6 (9-7) 6-3 6-4 ) ndani ya viwanja vya Melbourne Park nchini Australia

Djokovic mwenye miaka 35, alilazimika kufanyiwa matibabu juu ya maumivu ya misuli ya paja (hamstring) na kufungwa bandeji  kwenye mguu wake wa kushoto na sasa atapambana na Muastralia Alex de Minaur anayekamata nafasi ya 22 kwa viwango vya tenisi duniani kwa upande wa Wanaume