Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Ni nusu fainali ya kishindo Kombe la Mapinduzi

Jumanne , 10th Jan , 2017

Wapenzi na mashabiki wa soka visiwani Zanzibar leo wanataraji kupata burudani ya aina yake kwa kuwashudia watani wa jadi katika soka la Bongo Simba na Yanga wakipambana katika nusu fainali ya michuano ya Kombe la Mapinduzi inayoendelea visiwani humo

Wachezaji wa Yanga (juu) na wa Simba (chini)

 

Mchezo huo ambao ni wa pili ukipigwa majira ya saa 2:15 usiku, unataraji kuvuta hisia za wengi huku mamia ya mashabiki wakizidi kumiminika visiwani humo kutoka Tanzania Bara kwa ajili ya kushuhudia mtanange huo.

Yanga inaingia ikiwa na kumbukumbu ya kupigwa mabao 4-0 na Azam katika mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi huku ikijivunia kutoa kipigo kikubwa zaidi cha mabao 6-0 kwa Jamhuri ya Pemba, huku Simba ikijivunia kumaliza hatua ya makundi bila kupoteza mchezo licha ya kuonesha udhaifu katika safu yake ya ushambuliaji.

Kinachotia hamasa zaidi katika mchezo huo ni kitendo cha timu zote mbili kupeleka vikosi vyake kamili, ambavyo kwa ajili ya kulinda heshima, makocha wote watalazimika kupanga vikosi vyao imara zaidi katika mechi ya leo.

Takwimu zinaonesha kuwa katika mara 4 ambazo timu hizo zimekutana visiwani Zanzibar, Simba imeshinda mechi 3 huku Yanga ikishinda mechi 1 pekee, jambo ambalo linampa imani Msemaji wa Simba, Haji Manara ambaye amesema Simba ni lazima ishinde kutokana na kuwa na kikosi bora kuliko Yanga.

Mechi ya mwisho kwa Simba na Yanga kukutana visiwani humo na Simba kushinda 2-0

Kwa upande wa Yanga, wapenzi na mashabiki zake wametoa tambo kuwa ni lazima mnyama achinjwe kwa kuwa Simba haina kitu, na haina kikosi imara kama cha Yanga, huku wakijipa moyo kuwa kufungwa na Azam ilikuwa ni njia ya kutafuta hasira za kumuangamiza mnyama na wala hakuwastui.

Mchezo wa mwisho kwa timu hizo kukutana Zanzibar, Simba ilishinda mabao 2-0 kupitia kwa Mgosi na Shija Mkina.

Mchezo mwingine wa nusu fainali, utazikutanisha Azam FC, na Taifa Jang'ombe kuanzia saa 10:00 jioni.

Kikosi cha Azam FC katika mazoezi

HABARI ZAIDI

Mbunge wa Kilosa Profesa Palamagamba Kabudi

"Ndege ijayo ipewe jina la Mwl Nyerere" - Profesa

Baadhi ya Wanachi wa Kata ya Msowero, wakiwa Katika Mkutano wa Hadhara na Mkuu wa Wilaya

Mwenyekiti atiwa mbaroni kwa kuuza mlima, Msowero

Sehemu iliyokumbwa na Mafuriko Kusini mwa Brazil

Wanaokufa kutokana na mafuriko waongezeka Brazil

Baadhi ya Wabunge Wakichangia Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Uchukuzi

Serikali yashauriwa kuwa bunifu sekta ya usafiri

Baadhi ya Wananchi Wakishudia Ajali Iliyomgonga Mwendesha Bodaboda

Watatu wanusurika kifo, scania ikimgonga bodaboda

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Deogratius Ndejembi (kulia) pamoja na Meneja Mwandamizi wa Afya, Usalama na Mazingira kutoka GGML, Dk Kiva Mvungi (kushoto) wakimpatia vifaa kinga mmoja wa washiriki wa mafunzo kwa madereva bodaboda wa jiji la Arusha.

Bodaboda 200 Jijini Arusha wanolewa na kufundwa