Jumatatu , 28th Apr , 2014

Timu ya taifa ya ngumi za ridhaa ya Tanzania ambayo inajiwinda kwa mashindano ya Jumuiya ya Madola yatakayofanyika jijini Glascow nchini Scotland imeendelea na mazoezi makali kujiandaa kwa michuano hiyo.

mabondia wa timu ya taifa ya ngumi za ridhaa wakijifua

Timu ya taifa ya ngumi za ridhaa ya Tanzania ambayo inajiwinda kwa mashindano ya Jumuiya ya Madola yatakayofanyika jijini Glascow nchini Scotland imeendelea na mazoezi makali kujiandaa kwa michuano hiyo.

Timu hiyo pia timu hiyo inajipanga kwa safari ya nje ya nchi ambapo itakwenda kufanya mazoezi na mafunzo maalumu kwa ajili ya mashindano hayo.

Kocha msaidizi wa kikosi hicho Hassan Mzonge amesema maandalizi ya vijana wake tangu walipoanza wiki chache zilizopita yanatia moyo, na kutoa matumaini kuwa safari hii Watanzania wataibuka na medali katika michuano hiyo.

Aidha Mzonge amesema hali ya usikivu wa mafunzo na kujituma kwa mabondia itawasaidia katika mashindano hayo, na kwa sasa hali ya kikosi ni njema na wachezaji wataingia kambini jioni ya leo kwa ajili ya safari ya mafunzo nje ya nchi.