Jumatano , 29th Jun , 2016

Klabu ya Newcastle United imemsajili golikipa Matz Sels kutoka klabu ya KAA Gent kwa mkataba wa miaka 5.

Matz mwenye umri wa miaka 24 aliichezea timu ya vijana chini ya miaka 21 Ubelgiji na alisaidia klabu ya Gent kwa 2014-15 katika ligi ya Ubelgiji.

Golikipa huyo ambaye ndiye kipa bora wa mwaka kwa mwaka 2015 nchini Ubelgiji, amesema amefurahi sana kujiunga na klabu hiyo na kuwa uamuzi huo ni sahihi na rahisi.

Mpaka sasa klabu ya Newcastle ina makipa waandamizi wanne; Matz Sels, Karl Darlow, Tim Krul na Rob Elliot.

Krul alikosa kucheza michezo mingi katika msimu uliopita kutokana na majeraha na Elliot atakosa mechi za mwanzo za msimu ujao kutokana na tatizo la goti.

Chanzo BBC