Jumanne , 5th Jan , 2016

Mshambuliaji wa TP Mazembe, Mbwana Ally Samatta amesema kwasasa ndoa bado kabisa.

Mbwana Ally Samatta

"Nafikiri nitafanya hivyo pale nitakapokuwa nimetulia kidogo...kama nitakuwa ninacheza soka halitakuwa la ushindani sana wakati huo".

"Unajua maisha ya wanasoka ni kutangatanga hautulii kabisa. Ningependa kufunga ndoa katika kipindi ambacho nimetulia" alimalizia mchezaji huyo ambaye kwasasa ana miaka 23, akielekea 24.