Ijumaa , 16th Sep , 2022

Kiungo wa Singida Big Stars, Said Ndemla ameongezwa katika kikosi cha timu ya taifa, Taifa Stars kitakachocheza mechi mbili za kimataifa za kirafiki nchini Libya.

Kocha Mkuu wa Stars, Mzambia Hanour Janza amethibitisha kumuongeza Ndemla kutokana na ubora wake aliouonyesha kwenye siku za hivi karibuni.

“Tumeamua kumuongeza kutokana na ubora wake na huenda tukaongeza wengine na kufika Jumamosi mtajua kila kitu,” amesema Janza anayeinoa pia Namungo.

 

Tanzania itajitupa uwanjani Septemba 24, 2022 kucheza na Uganda na mechi ya mwisho itacheza na Libya Septemba 27 kisha kurudi Tanzania.

Michezo hiyo iliyo kwenye kalenda ya Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) zitakuwa na faida kwa makocha wa timu zote kimbinu na mipango hususani Taifa Stars na Uganda ambazo hapo baadae zitakutana kwenye mechi za kuwania kufuzu Afcon.

Ikumbukwe siku chache zilizopita, Taifa Stars ilishindwa kufuzu fainali za mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN)  kwa kutolewa na Uganda kwa jumla ya mabao 4-0 baada ya kufungwa 1-0 nyumbani na kuchapwa 3-0 ugenin