Jumatatu , 20th Oct , 2014

Wakati michuano ya Ligi Kuu Tanzania Bara ikizidi kushika kasi,timu ya Ndanda FC ya mjini Mtwara imemfukuza kocha wa timu hiyo Dennis Kitambi pamoja na kocha wa Magoli kipa Mohamed Mwarami.

Akizungumza na East Africa Radio, Seleman Kachele amesema wamefikia hatua hiyo baada ya uongozi kukaa kikao cha dharura na kujadili mambo mbalimbali yaliyopelekea timu hiyo kufungwa katika mechi zake za Ligi Kuu hivyo wakaamua kuchukua uamuzi huo.

Kachele amesema, timu hiyo itakuwa chini ya mkurugenzi wa Ufundi Mahibu Kanu mpaka pale watakapopata kocha wa kuchukua mikoba ya Kitambi na Mwarami.