Ijumaa , 21st Nov , 2014

Ratiba ya michuano ya Klabu bingwa Afrika ya Mpira wa Magongo wa wanawake inayoanza hapo Kesho nchini Zimbabwe inatarajiwa kutolewa leo jioni.

Katika taarifa ya Chama cha Mpira wa Magongo Afrika AHA,imesema ratiba ya michuano hiyo ilitarajiwa kutoka mapema leo lakini kutokana na timu mbili kujitoa katika mashindano hayo,imewalazimu kupanga ratiba nyingine ya michuabo hiyo.

Michuabo hiyo ilityarajiwa kushirikisha timu 10 kutoka nchi wanachama wa chama hicho,lakini kutokana na nchi mbili kutoshiriki michuano hiyo,timu nane ndizo zilizobaki katika ushiriki wa michuano hiyo inayoanza rasmi kesho na kumalizika Novemba 30 mwaka huu.