Alhamisi , 19th Feb , 2015

Mwenyekiti wa Chama cha Kriketi nchini TCA, Zurri Remtullaha amesema hali ya mchezo kwa nchi shiriki za michuano ya Afrika ya Kriketi kwa wanaume chini ya miaka 19 ni nzuri kutokana na kila timu kuwa na maandalizi ya kutosha.

Akizungumza na East Africa Radio, Remtullah amesema, Timu kutoka nchini Namibia imeonekana ilifanya maandalizi mapema na maandalizi yalikuwa mazuri kutokana na bidii waliyonayo katika mechi wanazocheza.

Remtullah amesema mpaka sasa timu ya Tanzania ina uwezo wa kufanya vizuri kama itafanya vizuri katika mechi zilizobakia na kujiwekea nafasi nzuri ya kufuzu kushiriki michuano ya Kriketi ya Kombe Dunia litakalofanyika mwakani Bangladesh. .

Timu kutoka Namibia, Nigeria, Botswana, Kenya,Uganda na wenyeji Tanzania inashiriki michuano hiyo, Jumatatu ijayo jijini Dar es Salaam ambapo inasimamiwa na marefa pamoja na kamishina wa mashindano kutoka nchini Afrika ya Kusini.