Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

#AUDIO Nahodha Isihaka apiga goti

Ijumaa , 18th Aug , 2017

Nahodha wa timu ya TMT, Isihaka Masoud ameomba radhi kwa utovu wa nidhamu aliyoonyesha katika mechi ya 'game 1' ya fainali za Sprite BBall Kings na kudai kilichotokea siku hiyo hakikuwa dhumuni lake ila hasira ndizo zilizomponza.

Nahodha wa timu ya TMT, Isihaka Masoud.

Isihaka amesema hayo leo baada ya kupita siku chache tokea alipofanya kitendo cha utovu wa nidhamu kwa kuwa tuhumu waamuzi 'Official' wa mchezo kuwa wanawabeba timu ya Mchenga BBall Stars kwa kuwa wao walifungwa kwa pointi 101-71 wakati alipokuwa akifanyiwa mahojiano 'Live' kupitia EATV uwanjani hapo jambo ambalo ni kinyume na sheria na taratibu za mchezo huo.

"Nimejisikia vibaya mwenyewe kwa kitendo nilichokifanya siku hiyo mpaka nafika nyumbani, nikawa najiuliza ni mimi kweli nimeongea yale maneno je watu watanifikiliaje?. Lakini naomba msamaha kwa washabiki wangu wote wa TMT, uongozi wa EATV, East Africa Radio, kwa mdhamini wa mashindano haya Sprite, TBF pamoja na watu wote wanaopenda mpira wa kikapu", alisema Isihaka.

Pamoja na hayo, Isihaka amesema kwa sasa amejifunza ni wapi anapaswa apeleke malalamiko yake pindi yanapotokea awapo uwanjani.

TMT inatarajiwa kushuka dimbani kesho kuvaana na Mchenga BBall Stars katika mchezo wa tatu wa fainali za Sprite BBall Kings katika viwanja vya Don Bosco Oysterbay Jijini Dar es Salaam majira ya saa tisa mchana kwa saa za Afrika Mashariki na Kati.

Msikilize hapa chini Nahodha wa TMT, Isihaka Masoud anavyoendelea kuongea zaidi.

HABARI ZAIDI

DCP David Misime, Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania

Mtoto atekwa na mzazi wake ili ajipatie milioni 20

Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Anton Sabasaba Akizungumza wakati alipohudhuria kikao cha wazazi katika Shule ya Msingi Elisabane Mei 24, 2024

Wototo wafuatiliwe na kulindwa kama mboni - Anton

Maduka ya Wafanyabiashara yakiwa yamefungwa

Wamiliki wa maduka Mebya wafunga biashara zao

Kamanda wa Polisi mkoa wa Songwe Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Agustino Senga

Polisi waambiwa kazi yao ni kazi ya Mungu

Kiwanda cha sukari Mtibwa

11 wafariki dunia kiwanda cha Mtibwa

Wilman Kapenjama Ndile, Mkuu wa Wilaya ya Songea

DC Kapenjama ataka uaminifu kwa wakulima Songea