
Picha ya mwanariadha Malaika Mihambo
Asili yake ya Tanzania inatokana na Baba yake mzazi, Mzee Mihambo ambaye ni mtu wa Zanzibar na mama yake ni Mjerumani ambapo kwa pamoja walibarikiwa kumpata Malaika Februari 3,1994 (27) huko Heidelberg, Ujerumani.
Rekodi zake kwenye mashindano ya riadha kimataifa kwa vijana mwaka 2011 alimaliza wa 9, huku 2013 alishinda medali ya dhahabu, mwaka 2016 katika Olimpiki pale Rio de Janeiro aliruka mita 6.95 na kushika nafsi ya nne, mwaka 2018 nafasi ya tano katika mashindano ya riadha ya ukumbini na kupata medali ya dhahabu na mwaka huu (2021) huko Tokyo kwenye Olimpiki amepata medali ya dhahabu.
Mihambo amesoma Heidelberg hadi kumaliza A-level, mwaka 2012 akajiunga na Chuo Kikuu cha Mannheim kusomea masuala ya elimu ya siasa na mwaka 2019 alianza kusoma elimu ya mazingira.