Jumatatu , 10th Aug , 2015

Winga Godfrey Mwashiuya ameiadhibu timu yake ya zamani, Kemondo kwa kuifunga mabao mawili katika ushindi wa 4-1 hapo jana Uwanja wa CCM Mbozi, Mbeya.

Mshambuliaji wa Yanga, Geofrey Mwashiuya akimtoka beki wa KMKM, Kassim Abdulkadir

Yanga SC ilikwenda kupumzika ikiwa nyuma kwa bao 1-0, lakini kipindi cha pili kocha Mholanzi, Hans van der Pluijm akabadilisha kikosi na timu ikapindua matokeo ambapo beki Juma Abdul alimpisha Mbuyu Twite, kiungo Thabani Kamusoko akampisha Said Juma ‘Makapu’, winga Deus Kaseke akampisha Mwashiuya na mshambuliaji Malimi Busungu akampisha Amisi Tambwe.

Mwashiuya aliyesajiliwa Yanga SC msimu huu kutoka Kemondo, akafunga mabao mawili, Simon Msuva na Tambwe moja yaliyopelekea mchezo huo kumalizika kwa Yanga kuibuka na ushindi wa 4-1.

Yanga SC inaondoka Mbozi mara baada ya mchezo tu, kuelekea Tukuyu mkoani Mbeya pia, kuweka kambi ya kujiandaa na mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Azam FC Agosti 22, mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.