Mchezo wa Simba dhidi ya Yanga utachezwa Saa 11:00 jioni
Emmanuel Mwandembwa kutoka Arusha ndio atakaye kuwa mwamuzi wa kati kwenye mchezo huo wa kiporo mchezo namba 208 wa VPL utakaoanza kutimua vumbi Saa 11:00 Jioni, ambapo atasaidiwa na mwamuzi msaidizi namba moja Frank Komba wa Dar es salaam, mwamuzi msaidizi namba mbili Hamdan Said wa Mtwara na mwamuzi namba nne ni Ramadhani Kayoko wa Dar es salaam.
Hii hapa orodha kamili ya maofisa watakao simamia mchezo huo wa watani wa jadi wa soka la Tanznaia Simba na Yanga.

