Mwanariadha wa Uganda Rebecca Cheptegei amefariki Dunia leo Septemba 5, 2024.
Mwariadha huyo amefariki kutokana na majeraha hayo ya moto, ambapo Septemba 2, 2024 Kamanda wa polisi wa Kaunti ya Trans-Nzoia Jeremiah ole Kosiom alisema mwenza wa zamani wa mwanariadha huyo Dickson Ndiema, alinunua petroli, akammiminia na kumchoma moto Rebecca Cheptegei.
Cheptegei amefariki Dunia akiwa na umri wa miaka 33 na alikuwa sehemu ya wanariadha walioshiriki michezo ya Olimpikin ya majaira ya joto iliyofanyiaka Paris nchini Ufaransa na alimaliza nafasi ya 44 kwenye mbio za marathon. Na Rais wa Kamati ya Olimpiki ya Uganda Donald Rukare ametuma salamu za rambirambi kufuatia kifo mwanariadha huyo.