Alhamisi , 28th Sep , 2023

Bondia Hassan Mwakinyo amesema kesho hatapanda Ulingoni kupigana dhidi ya Bondia Julius Indonga kwenye pambano la kuwania mkanda wa IBA International. Amesema hatapigana kutogana na Uwongo na Udanganyifu wa Ma Promota.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika kuwa "Binafsi!! Napenda sana Kushukuru M/mungu kwa uzima na Afya nilio nayo Leo” pia niwashukuru sana washabiki zangu kwa kujitokeza kwa Nguvu kuonyesha shauku ya kuni support nawashukuru sana AZAM TV kwa kuendelea kutoa nafasi!! Kwetu kama wachezaji wa ndani naomba niweke hisia zangu wazi kwa mashabiki ya kuwa kesho sitaweza kupanda ulingoni kutokana na uwongo na udanganyifu, wa ma promota binafsi sina tatizo na Mtu ila pia naheshimu sana kazi yangu na siko tayari kuona watu wana nijaribu au kutaka kuarbu jina langu Azam nia na dhamira yenu ni njema sana kwenye mchezo wa ngumi na kwa nidhamu ya juu kabisa maamuzi ya hili kuendelea yako mikononi kwenu hapa tulipofkia nyinyi binafsi ndio mnaweza kutatua hii changamoto na Muda ni Leo tu " Amesema Mwakinyo