Alhamisi , 10th Nov , 2016

Rais wa Uganda, Yoweri Kaguta Museveni amewapa mwaliko wa chakula cha mchana leo, wachezaji wa timu ya Taifa ya Uganda maarufu kama Uganda Cranes, wanaojiandaa na mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia mwaka 2018 dhidi ya Congo Brazzaville, Jumamosi hii.

Rais Museven akiwa na Timu ya Taifa ya Uganda "The Cranes"

 

Mkuu wa Mawasiliano wa Shirikisho la Soka nchini Uganda FUFA, Ahmed Hussein, amethibitisha taarifa hiyo, ambapo wachezaji wote walio kambini, maafisa na ujumbe wa FUFA, atajumuika na Rais Museveni kwenye Ikulu yake kwa chakula cha mchana.

Kocha wa timu ya soka ya Uganda, Milutin Sredejovic amesema anaamini mwaliko wa Ikulu ya Rais utaongeza morali ya wachezaji kushinda mchezo huo wa Jumamosi wa kufuzu Kombe la Dunia, dhidi ya Congo Brazzaville.

Rais Museveni alishawahi kuwapa mwaliko wachezaji wa The Cranes, kwenye Ikulu ya Entebbe mwaka uliopita, baada ya kushinda taji la Mataifa ya Afrika Mashariki na kati CECAFA Senior Challenge 2015, nchini Ethiopia.