Katibu Mkuu wa MTWAREFA Charles George amesema, tukio hilo lilitokea kwa upande wa timu moja shiriki ya michuano hiyo ya Super Eagles ambapo baada ya ukaguzi wa timu karatasi ya majina ya timu hiyo iliwakilishwa mezani kwa mwamuzi wa akiba ikiwa na pesa ambapo kiongozi wa timu pinzani alihisi na kutoa taarifa.
George amesema, baada ya kuchunguza waligundua kuwa ni pesa zilizopelekwa pamoja na karatasi ya majina ambapo mpaka hivi sasa hawajajua pesa hizo zilipelekwa na nani.
George amesema, baada ya tukio hilo walikubaliana kukutana ili kamati iweze kutoa kauli ya mwisho kwa mujibu wa kanuni na kama ni adhabu watazitoa kutokana na kanuni zinavyowaelekeza kutokana na kosa kama hilo.





