Mwanariadha wa Tanzania Alphonce Felix Simbu amemaliza nafasi ya 17 kwenye mbio ndefu za marathon Kilomita 42 kwenye michezo ya Olimpiki.
Mwanariadha mwingine wa Tanzania upande wa wanaume Gabriel Geay ameshindwa kumaliza mbio hizo.
Mshindi wa mbio hizi ni Tamirat Tola kutoka nchini Ethiopia amemaliza mbio hizo ndani ya Masaa 2:06:26 akiivunja rekodi ya mkenya Samuel Wanjiru ya mwaka 2008, Wanjiru alikimbia kwa masaa 2:06:32.