Akizungumza jijini Dar es salaam, Afisa habari wa TFF, Baraka Kizuguto amesema, hatua hiyo imefikiwa na Kamati ya Utendaji kutokana na sababu za kutokukamilika kwa miundombinu ya mkutano mkuu na kuwepo kwa shughuli nyingine za kijamii mkoani humo.
Kamati ya Utendaji inamshukuru Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu mkoa wa Singida SIREFA, na uongozi mzima kwa kujitolea kuandaa mkutano huo na huko nyuma waliweza kuandaa mkutano wa makatibu wa vyama vya soka vya mikoa.
Kizuguto amesema, TFF itaandaa vikao na matukio mengine mkoani Singida itakapotokea hapo baadaye, tarehe ya mkutano mkuu itaendelea kubakia ile ile ya Machi 14, 15 mwaka huu.
