Kocha wa Mji Njombe ambae zamani alikua akiifundisha timu ya Prison ya Jijini Mbeya alipokuwa hospitali Muhimbili hivi karibuni.
Akzingumza na East Africa Radio msemaji timu hiyo Solanus Mhagama amesema Mwamwaja amendelea kupata nafuu lakini kwa sasa ni mapema mno kurejea kazini na hivi sasa kocha msaidizi Boniface Damian ndiye anayeendelea kukinoa kikosi chao.
Mhagama amesisitiza kuwa licha ya kumkosa mwamwaja wanaimani wataendelea kufanya vyema kwenye michuano ya ligi daraja la kwanza na ile ya kombe la FA ambapo watakipiga na Green Warrious ya jijini Dar es salaam desemba 24 mwaka huu katika uwanja wa Amani Makambako.
Mji njombe wanashika nafasi ya Pili kwenye kundi B la ligi daraja la kwanza wakiwa na pointi 13 huku kinara wa kundi hilo ni masarange wa Ruvu Shooting ya mkoani Pwani wenye pointi 16.