Bondia Francis Miyeyusho (Kushoto) na Mohamed Matumla (Kulia)
Mabondia Francis Miyeyusho na Mohamed Matumla hii leo wamepima uzito na afya zao tayari kwa mpambano wao wa raundi kumi kuwania ubingwa wa kimataifa wa UBO mpambano utakaofanyika kesho jijini Dar es salaam.
Pambano hilo litasimamiwa na Organization ya ngumi za kulipwa Tanzania TPBO ambapo Rais wake Yasin Abdallah ustaadh ametoa ufafanuzi juu ya kwanini mpambano huo uwe wa uzito wa unyoya [feza] kilo 57 badala ya awali kuwa bantam kilo 55, ambapo amesema sababu kubwa ni vipimo walivyofanyiwa wote wawili kukutwa vikiwa vimeongezeka na kufikia Kilo 57.
kwa upande wao mabondia Mohamed Matumla na Francis Miyeyusho kila mmoja ametamba kuibuka na ushindi hapo kesho lakini walijibizana kuhusu matumizi ya dawa za kuongeza nguvu kauli ambayo aliianzisha Matumla akitaka wapimwe kabla na baada ya mpambano huo.
Naye mratibu wa mpambano huo Ally Mwanzowa amewataka mabondia hao kucheza mchezo wa kiungwana na kuleta burudani na kumsihi Mohamed Matumla asimdharau Miyeyusho kutokana na kupoteza mpambano wake uliopita dhidi ya bondia kutoka Thailand