Alhamisi , 12th Mei , 2022

Licha ya kuwa na msimu mbaya ,shambuliaji wa Klabu ya PSG ya Ufaransa, Lionel Messi ndiye mwanamichezo anayelipwa pesa zaidi ulimwenguni kwa kipindi cha miezi 12 iliyopita na hii ni kwa mujibu wa jarida la Forbes.

Lionel Messi katika majukumu yake dimbani

Messi mwenye umri wa miaka 34 ameripotiwa kujikusanyia dola milioni 130 kwa Mwaka kutokana na shughuli za uwanjani na hivyo kumfanya kuwa mbele ya LeBron James na mpinzani wake wa zamani Cristiano Ronaldo.

Messi ambaye anavuna dola milioni 75 kwa mwaka kutokana na soka, pia hupokea dola milioni 55 kutokana na mikataba ya udhamini na ridhaa.

Hii ni kwa mara ya pili muafgentina huyo kukaa juu ya orodha ya Forbes ambapo mara ya mwisho kufanya hivyo ilikuwa mwaka 2019.

Wanamichezo 10 ambao wote ni wanaume wamejikusanyia dola milioni 992 kwa miezi 12 iliyopita katika mapato ya jumla kabla ya kodi.

 

Ifuatayo ni orodha ya wanamichezo 10 waliojikusanyia pesa zaidi kwa mwaka 2022.

1-Lionel Messi-dola milioni 130

2-LeBron James-dola milioni 121

3-Cristiano Ronaldo-dola milioni 115

4-Neymar Jr-dola milioni 95

5-Stephen Curry-dola milioni 92.8

6-Kevin Durant-dola milioni 90.1

7-Roger Federer-dola milioni 90.7

8-Canelo Alvarez-dola milioni 90